Native Bible

Genesis 49:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi,* yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.

Genesis 49:25 in English

Genesis 49:25 · Berean Standard Bible

by the God of your father who helps you, and by the Almighty * who blesses you, with blessings of the heavens above, with blessings of the depths below, with blessings of the breasts and womb.

Context

23Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. 24Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, 25kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi,* yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi. 26Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 27“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.