Mwanzo 49:27
Genesis 49:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”
Genesis 49:27 in English
Genesis 49:27 · Berean Standard Bible
Benjamin is a ravenous wolf; in the morning he devours the prey, in the evening he divides the plunder.”
Context
25kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,
kwa sababu ya Mwenyezi,* yeye anayekubariki
kwa baraka za mbinguni juu,
baraka za kilindi kilichoko chini,
baraka za matitini na za tumbo la uzazi. 26Baraka za baba yako ni kubwa
kuliko baraka za milima ya kale,
nyingi kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 27“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;
asubuhi hurarua mawindo yake,
jioni hugawa nyara.” 28Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa. 29Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.