Mwanzo 49:28
Genesis 49:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.
Genesis 49:28 in English
Genesis 49:28 · Berean Standard Bible
These are the tribes of Israel, twelve in all, and this was what their father said to them. He blessed them, and he blessed each one with a suitable blessing.
Context
26Baraka za baba yako ni kubwa
kuliko baraka za milima ya kale,
nyingi kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 27“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;
asubuhi hurarua mawindo yake,
jioni hugawa nyara.” 28Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa. 29Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, 30pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.