Mwanzo 49:24
Genesis 49:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,
Genesis 49:24 in English
Genesis 49:24 · Berean Standard Bible
Yet he steadied his bow, and his strong arms were tempered by the hands of the Mighty One of Jacob, in the name of the Shepherd, the Rock of Israel,
Context
22“Yosefu ni mzabibu uzaao,
mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi,
ambao matawi yake hutanda ukutani. 23Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia,
wakampiga mshale kwa ukatili. 24Lakini upinde wake ulibaki imara,
mikono yake ikatiwa nguvu,
na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,
kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, 25kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,
kwa sababu ya Mwenyezi,* yeye anayekubariki
kwa baraka za mbinguni juu,
baraka za kilindi kilichoko chini,
baraka za matitini na za tumbo la uzazi. 26Baraka za baba yako ni kubwa
kuliko baraka za milima ya kale,
nyingi kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.