Native Bible

Genesis 30:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.”

Genesis 30:26 in English

Genesis 30:26 · Berean Standard Bible

Give me my wives and children for whom I have served you, that I may go on my way. You know how hard I have worked for you.”

Context

24Akamwita Yosefu* na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.” 25Baada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu. 26Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.” 27Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba Bwana amenibariki kwa sababu yako.” 28Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.