Native Bible

Genesis 30:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.”

Genesis 30:28 in English

Genesis 30:28 · Berean Standard Bible

And he added, “Name your wages, and I will pay them.”

Context

26Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.” 27Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba Bwana amenibariki kwa sababu yako.” 28Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.” 29Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi ambavyo nimekutumikia na jinsi ambavyo wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu. 30Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, naye Bwana amekubariki popote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.