Mwanzo 19:24
Genesis 19:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa Bwana juu ya Sodoma na Gomora.
Genesis 19:24 in English
Genesis 19:24 · Berean Standard Bible
Then the LORD rained down sulfur and fire on Sodom and Gomorrah—from the LORD out of the heavens.
Context
22Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.*) 23Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. 24Ndipo Bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa Bwana juu ya Sodoma na Gomora. 25Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi. 26Lakini mke wa Loti akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.