Mwanzo 11:10
Genesis 11:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.
Genesis 11:10 in English
Genesis 11:10 · Berean Standard Bible
This is the account of Shem. Two years after the flood, when Shem was 100 years old, he became the father of Arphaxad.
Context
8Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 9Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote. 10Hivi ndivyo vizazi vya Shemu.
Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi. 11Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 12Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.