Native Bible

Ezekiel 28:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, wewe una hekima kuliko Danieli? Je, hakuna siri iliyofichika kwako?

Ezekiel 28:3 in English

Ezekiel 28:3 · Berean Standard Bible

Behold, you are wiser than Daniel; no secret is hidden from you!

Context

1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna na umesema, “Mimi ni mungu; nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu katika moyo wa bahari.” Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu. 3Je, wewe una hekima kuliko Danieli? Je, hakuna siri iliyofichika kwako? 4Kwa hekima yako na ufahamu wako, umejipatia utajiri, nawe umejikusanyia dhahabu na fedha katika hazina zako. 5Kwa werevu wako mwingi katika biashara, umeongeza utajiri wako na kwa sababu ya utajiri wako moyo wako umekuwa na kiburi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.