Ezekieli 28:4
Ezekiel 28:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hekima yako na ufahamu wako, umejipatia utajiri, nawe umejikusanyia dhahabu na fedha katika hazina zako.
Ezekiel 28:4 in English
Ezekiel 28:4 · Berean Standard Bible
By your wisdom and understanding you have gained your wealth and amassed gold and silver for your treasuries.
Context
2“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna
na umesema, “Mimi ni mungu;
nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu
katika moyo wa bahari.”
Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,
ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu. 3Je, wewe una hekima kuliko Danieli?
Je, hakuna siri iliyofichika kwako? 4Kwa hekima yako na ufahamu wako,
umejipatia utajiri,
nawe umejikusanyia dhahabu
na fedha katika hazina zako. 5Kwa werevu wako mwingi katika biashara,
umeongeza utajiri wako
na kwa sababu ya utajiri wako
moyo wako umekuwa na kiburi. 6“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,
mwenye hekima kama mungu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.