Ezekieli 28:5
Ezekiel 28:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa werevu wako mwingi katika biashara, umeongeza utajiri wako na kwa sababu ya utajiri wako moyo wako umekuwa na kiburi.
Ezekiel 28:5 in English
Ezekiel 28:5 · Berean Standard Bible
By your great skill in trading you have increased your wealth, but your heart has grown proud because of it.
Context
3Je, wewe una hekima kuliko Danieli?
Je, hakuna siri iliyofichika kwako? 4Kwa hekima yako na ufahamu wako,
umejipatia utajiri,
nawe umejikusanyia dhahabu
na fedha katika hazina zako. 5Kwa werevu wako mwingi katika biashara,
umeongeza utajiri wako
na kwa sababu ya utajiri wako
moyo wako umekuwa na kiburi. 6“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,
mwenye hekima kama mungu, 7mimi nitawaleta wageni dhidi yako,
taifa katili kuliko yote;
watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,
na kuchafua fahari yako inayongʼaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.