Native Bible

Ezekiel 27:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari itokayo Seniri;* walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti.

Ezekiel 27:5 in English

Ezekiel 27:5 · Berean Standard Bible

They constructed all your planking with cypress * from Senir.* They took a cedar from Lebanon to make a mast for you.

Context

3Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ee Tiro, wewe umesema, “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” 4Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. 5Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari itokayo Seniri;* walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. 6Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha* yako na kuipamba kwa pembe za ndovu. 7Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako, nacho kilikuwa bendera yako; chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau kutoka visiwa vya Elisha.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.