Ezekieli 27:3
Ezekiel 27:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ee Tiro, wewe umesema, “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”
Ezekiel 27:3 in English
Ezekiel 27:3 · Berean Standard Bible
Tell Tyre, who dwells at the gateway to the sea, merchant of the peoples on many coasts, that this is what the Lord GOD says: You have said, O Tyre, ‘I am perfect in beauty.’
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. 3Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,
“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” 4Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,
wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. 5Walizifanya mbao zako zote
kwa misunobari itokayo Seniri;*
walichukua mierezi kutoka Lebanoni
kukutengenezea mlingoti.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.