Ezekieli 27:4
Ezekiel 27:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.
Ezekiel 27:4 in English
Ezekiel 27:4 · Berean Standard Bible
Your borders are in the heart of the seas; your builders perfected your beauty.
Context
2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. 3Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,
“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” 4Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,
wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. 5Walizifanya mbao zako zote
kwa misunobari itokayo Seniri;*
walichukua mierezi kutoka Lebanoni
kukutengenezea mlingoti. 6Walichukua mialoni toka Bashani
wakakutengenezea makasia yako;
kwa miti ya msanduku
kutoka pwani ya Kitimu
wakatengeneza sitaha* yako
na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.