Ezekieli 27:6
Ezekiel 27:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha* yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Ezekiel 27:6 in English
Ezekiel 27:6 · Berean Standard Bible
Of oaks from Bashan they made your oars; of wood from the coasts of Cyprus * they made your deck, inlaid with ivory.
Context
4Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,
wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. 5Walizifanya mbao zako zote
kwa misunobari itokayo Seniri;*
walichukua mierezi kutoka Lebanoni
kukutengenezea mlingoti. 6Walichukua mialoni toka Bashani
wakakutengenezea makasia yako;
kwa miti ya msanduku
kutoka pwani ya Kitimu
wakatengeneza sitaha* yako
na kuipamba kwa pembe za ndovu. 7Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,
nacho kilikuwa bendera yako;
chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau
kutoka visiwa vya Elisha. 8Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;
watu wako wenye ustadi, ee Tiro,
walikuwa ndio mabaharia wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.