Native Bible

Ezekiel 27:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nchi za pwani zitatetemeka wakati mabaharia wako watakapopiga kelele.

Ezekiel 27:28 in English

Ezekiel 27:28 · Berean Standard Bible

The countryside will shake when your sailors cry out.

Context

26Wapiga makasia wako wanakupeleka mpaka kwenye maji makavu. Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande katika moyo wa bahari. 27Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote, na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako. 28Nchi za pwani zitatetemeka wakati mabaharia wako watakapopiga kelele. 29Wote wapigao makasia wataacha meli zao, mabaharia wote na wanamaji wote watasimama pwani. 30Watapaza sauti zao na kulia sana kwa ajili yako; watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao na kujivingirisha kwenye majivu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.