Native Bible

Ezekiel 27:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wote wapigao makasia wataacha meli zao, mabaharia wote na wanamaji wote watasimama pwani.

Ezekiel 27:29 in English

Ezekiel 27:29 · Berean Standard Bible

All who handle the oars will abandon their ships. The sailors and all the captains of the sea will stand on the shore.

Context

27Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote, na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako. 28Nchi za pwani zitatetemeka wakati mabaharia wako watakapopiga kelele. 29Wote wapigao makasia wataacha meli zao, mabaharia wote na wanamaji wote watasimama pwani. 30Watapaza sauti zao na kulia sana kwa ajili yako; watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao na kujivingirisha kwenye majivu. 31Watanyoa nywele zao kwa ajili yako, nao watavaa nguo za magunia. Watakulilia kwa uchungu wa moyo na kwa maombolezo makuu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.