Ezekieli 27:27
Ezekiel 27:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote, na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako.
Ezekiel 27:27 in English
Ezekiel 27:27 · Berean Standard Bible
Your wealth, wares, and merchandise, your sailors, captains, and shipwrights, your merchants and all the warriors within you, with all the other people on board, will sink into the heart of the sea on the day of your downfall.
Context
25“ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo
zinazokusafirishia bidhaa zako.
Umejazwa shehena kubwa
katika moyo wa bahari. 26Wapiga makasia wako wanakupeleka
mpaka kwenye maji makavu.
Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande
katika moyo wa bahari. 27Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako,
mabaharia wako, manahodha wako,
mafundi wako wa meli,
wafanyabiashara wako na askari wako wote,
na kila mmoja aliyeko melini
atazama kwenye moyo wa bahari
siku ile ya kuvunjika kwa meli yako. 28Nchi za pwani zitatetemeka
wakati mabaharia wako watakapopiga kelele. 29Wote wapigao makasia
wataacha meli zao,
mabaharia wote na wanamaji wote
watasimama pwani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.