Ezekieli 23:32
Ezekiel 23:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; nitaletea juu yako dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana.
Ezekiel 23:32 in English
Ezekiel 23:32 · Berean Standard Bible
This is what the Lord GOD says: ‘You will drink your sister’s cup, a cup deep and wide. It will bring scorn and derision, for it holds so much.
Context
30umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao. 31Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako. 32“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“Utakinywea kikombe cha dada yako,
kikombe kikubwa na chenye kina kirefu;
nitaletea juu yako dharau na dhihaka,
kwa kuwa kimejaa sana. 33Utalewa ulevi na kujawa huzuni,
kikombe cha maangamizo na ukiwa,
kikombe cha dada yako Samaria. 34Utakinywa chote na kukimaliza;
utakivunja vipande vipande
na kuyararua matiti yako.
Nimenena haya, asema Bwana Mwenyezi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.