Native Bible

Ezekiel 23:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.

Ezekiel 23:31 in English

Ezekiel 23:31 · Berean Standard Bible

Because you have followed the path of your sister, I will put her cup into your hand.’

Context

29Watakushughulikia kwa chuki na kukunyangʼanya kila kitu ulichokifanyia kazi. Watakuacha uchi na mtupu na aibu ya ukahaba wako itafunuliwa. Uasherati wako na uzinzi wako 30umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao. 31Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako. 32“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; nitaletea juu yako dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana. 33Utalewa ulevi na kujawa huzuni, kikombe cha maangamizo na ukiwa, kikombe cha dada yako Samaria.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.