Ezekieli 21:30
Ezekiel 21:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Urudishe upanga kwenye ala yake! Katika mahali ulipoumbiwa, katika nchi ya baba zako, huko nitakuhukumu.
Ezekiel 21:30 in English
Ezekiel 21:30 · Berean Standard Bible
Return the sword to its sheath! In the place where you were created, in the land of your origin, I will judge you.
Context
28“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao.
“ ‘Upanga, upanga,
umefutwa kwa ajili ya kuua,
umesuguliwa ili kuangamiza
na unametameta kama umeme wa radi! 29Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako,
wanapobashiri uongo kwa ajili yako,
wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu,
wale walio waovu,
wale ambao siku yao imewadia,
wakati wa adhabu yao ya mwisho. 30Urudishe upanga kwenye ala yake!
Katika mahali ulipoumbiwa,
katika nchi ya baba zako,
huko nitakuhukumu. 31Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako
na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako;
nitakutia mikononi mwa watu wakatili,
watu stadi katika kuangamiza. 32Mtakuwa kuni za kuwashia moto,
damu yenu itamwagwa katika nchi yenu,
wala hamtakumbukwa tena;
kwa maana Mimi Bwana nimesema.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.