Ezekieli 21:28
Ezekiel 21:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao. “ ‘Upanga, upanga, umefutwa kwa ajili ya kuua, umesuguliwa ili kuangamiza na unametameta kama umeme wa radi!
Ezekiel 21:28 in English
Ezekiel 21:28 · Berean Standard Bible
Now prophesy, son of man, and declare that this is what the Lord GOD says concerning the Ammonites and their contempt: ‘A sword! A sword is drawn for slaughter, polished to consume, to flash like lightning—
Context
26hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa na aliyekwezwa atashushwa. 27Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya mpaka aje yule ambaye ndiye mwenye haki nao; yeye ndiye nitakayempa.’ 28“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao.
“ ‘Upanga, upanga,
umefutwa kwa ajili ya kuua,
umesuguliwa ili kuangamiza
na unametameta kama umeme wa radi! 29Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako,
wanapobashiri uongo kwa ajili yako,
wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu,
wale walio waovu,
wale ambao siku yao imewadia,
wakati wa adhabu yao ya mwisho. 30Urudishe upanga kwenye ala yake!
Katika mahali ulipoumbiwa,
katika nchi ya baba zako,
huko nitakuhukumu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.