Ezekieli 21:32
Ezekiel 21:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtakuwa kuni za kuwashia moto, damu yenu itamwagwa katika nchi yenu, wala hamtakumbukwa tena; kwa maana Mimi Bwana nimesema.’ ”
Ezekiel 21:32 in English
Ezekiel 21:32 · Berean Standard Bible
You will be fuel for the fire. Your blood will stain your own land. You will not be remembered, for I, the LORD, have spoken.’”
Context
30Urudishe upanga kwenye ala yake!
Katika mahali ulipoumbiwa,
katika nchi ya baba zako,
huko nitakuhukumu. 31Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako
na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako;
nitakutia mikononi mwa watu wakatili,
watu stadi katika kuangamiza. 32Mtakuwa kuni za kuwashia moto,
damu yenu itamwagwa katika nchi yenu,
wala hamtakumbukwa tena;
kwa maana Mimi Bwana nimesema.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.