Native Bible

Exodus 30:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,* na kimo cha dhiraa mbili,* nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo.

Exodus 30:2 in English

Exodus 30:2 · Berean Standard Bible

It is to be square, a cubit long, a cubit wide, and two cubits high.* Its horns must be of one piece.

Context

1“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 2Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,* na kimo cha dhiraa mbili,* nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. 3Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. 4Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.