Native Bible

Exodus 30:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu.

Exodus 30:4 in English

Exodus 30:4 · Berean Standard Bible

And make two gold rings below the molding on opposite sides to hold the poles used to carry it.

Context

2Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,* na kimo cha dhiraa mbili,* nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. 3Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. 4Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu. 5Tengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu. 6Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.