Native Bible

Exodus 30:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana.

Exodus 30:14 in English

Exodus 30:14 · Berean Standard Bible

Everyone twenty years of age or older who crosses over must give this offering to the LORD.

Context

12“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 13Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana. 14Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana. 15Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. 16Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.