Kutoka 30:15
Exodus 30:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu.
Exodus 30:15 in English
Exodus 30:15 · Berean Standard Bible
In making the offering to the LORD to atone for your lives, the rich shall not give more than a half shekel, nor shall the poor give less.
Context
13Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana. 14Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana. 15Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. 16Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.” 17Kisha Bwana akamwambia Mose,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.