Native Bible

Exodus 30:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana.

Exodus 30:13 in English

Exodus 30:13 · Berean Standard Bible

Everyone who crosses over to those counted must pay a half shekel,* according to the sanctuary shekel, which weighs twenty gerahs.* This half shekel is an offering to the LORD.

Context

11Naye Bwana akamwambia Mose, 12“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 13Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana. 14Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana. 15Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.