Native Bible

Exodus 30:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye Bwana akamwambia Mose,

Exodus 30:11 in English

Exodus 30:11 · Berean Standard Bible

Then the LORD said to Moses,

Context

9Usifukize uvumba mwingine wowote juu ya madhabahu haya au sadaka nyingine yoyote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake. 10Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Bwana.” 11Naye Bwana akamwambia Mose, 12“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 13Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.