Native Bible

Exodus 30:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu.

Exodus 30:12 in English

Exodus 30:12 · Berean Standard Bible

“When you take a census of the Israelites to number them, each man must pay the LORD a ransom for his life when he is counted. Then no plague will come upon them when they are numbered.

Context

10Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Bwana.” 11Naye Bwana akamwambia Mose, 12“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 13Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana. 14Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.