Kutoka 15:4
Exodus 15:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Magari ya vita ya Farao na jeshi lake amewatosa baharini. Maafisa wa Farao walio bora sana wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.
Exodus 15:4 in English
Exodus 15:4 · Berean Standard Bible
Pharaoh’s chariots and army He has cast into the sea; the finest of his officers are drowned in the Red Sea.*
Context
2Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,
Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3Bwana ni shujaa wa vita;
Bwana ndilo jina lake. 4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake
amewatosa baharini.
Maafisa wa Farao walio bora sana
wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. 5Maji yenye kina yamewafunika,
wamezama mpaka vilindini kama jiwe. 6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana
ulitukuka kwa uweza.
Mkono wako wa kuume, Ee Bwana,
ukamponda adui.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.