Native Bible

Exodus 15:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, ukamponda adui.

Exodus 15:6 in English

Exodus 15:6 · Berean Standard Bible

Your right hand, O LORD, is majestic in power; Your right hand, O LORD, has shattered the enemy.

Context

4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake amewatosa baharini. Maafisa wa Farao walio bora sana wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. 5Maji yenye kina yamewafunika, wamezama mpaka vilindini kama jiwe. 6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, ukamponda adui. 7Katika ukuu wa utukufu wako, ukawaangusha chini wale waliokupinga. Uliachia hasira yako kali, ikawateketeza kama kapi. 8Kwa pumzi ya pua zako maji yalijilundika. Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.