Native Bible

Exodus 15:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika ukuu wa utukufu wako, ukawaangusha chini wale waliokupinga. Uliachia hasira yako kali, ikawateketeza kama kapi.

Exodus 15:7 in English

Exodus 15:7 · Berean Standard Bible

You overthrew Your adversaries by Your great majesty. You unleashed Your burning wrath; it consumed them like stubble.

Context

5Maji yenye kina yamewafunika, wamezama mpaka vilindini kama jiwe. 6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, ukamponda adui. 7Katika ukuu wa utukufu wako, ukawaangusha chini wale waliokupinga. Uliachia hasira yako kali, ikawateketeza kama kapi. 8Kwa pumzi ya pua zako maji yalijilundika. Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9“Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwa wao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.