Kutoka 15:2
Exodus 15:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
Exodus 15:2 in English
Exodus 15:2 · Berean Standard Bible
The LORD is my strength and my song, and He has become my salvation. He is my God, and I will praise Him, my father’s God, and I will exalt Him.
Context
1Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu:
“Nitamwimbia Bwana,
kwa kuwa ametukuzwa sana.
Farasi na mpanda farasi
amewatosa baharini. 2Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,
Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3Bwana ni shujaa wa vita;
Bwana ndilo jina lake. 4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake
amewatosa baharini.
Maafisa wa Farao walio bora sana
wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.