Native Bible

Exodus 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana ni shujaa wa vita; Bwana ndilo jina lake.

Exodus 15:3 in English

Exodus 15:3 · Berean Standard Bible

The LORD is a warrior, the LORD is His name.

Context

1Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu: “Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini. 2Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3Bwana ni shujaa wa vita; Bwana ndilo jina lake. 4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake amewatosa baharini. Maafisa wa Farao walio bora sana wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. 5Maji yenye kina yamewafunika, wamezama mpaka vilindini kama jiwe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.