Mhubiri 8:3
Ecclesiastes 8:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lolote apendalo.
Ecclesiastes 8:3 in English
Ecclesiastes 8:3 · Berean Standard Bible
Do not hasten to leave his presence, and do not persist in a bad cause, for he will do whatever he pleases.
Context
1Ni nani aliye kama mtu mwenye hekima?
Ni nani ajuaye maelezo ya mambo?
Hekima hungʼarisha uso wa mtu na kubadili ugumu wa uso wake. 2Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. 3Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lolote apendalo. 4Kwa kuwa neno la mfalme ndilo lenye mamlaka ya mwisho, nani awezaye kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?” 5Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika,
moyo wa hekima utajua wakati muafaka
na jinsi ya kutenda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.