Native Bible

Ecclesiastes 12:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.

Ecclesiastes 12:7 in English

Ecclesiastes 12:7 · Berean Standard Bible

before the dust returns to the ground from which it came and the spirit returns to God who gave it.

Context

5wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu na hatari zitakazokuwepo barabarani; wakati mlozi utakapochanua maua na panzi kujikokota nawe usiwe na shauku ya kitu chochote. Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele nao waombolezaji wakizunguka barabarani. 6Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha, au bakuli la dhahabu halijavunjika; kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi, au gurudumu kuvunjika kisimani, 7nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa. 8Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili! Kila kitu ni ubatili!” 9Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.