Native Bible

Deuteronomy 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Si kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo.

Deuteronomy 5:3 in English

Deuteronomy 5:3 · Berean Standard Bible

He did not make this covenant with our fathers, but with all of us who are alive here today.

Context

1Mose akawaita Israeli wote, akawaambia: Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 2Bwana Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 3Si kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 4Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.