Kumbukumbu 32:9
Deuteronomy 32:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa fungu la Bwana ni watu wake, Yakobo kura yake ya urithi.
Deuteronomy 32:9 in English
Deuteronomy 32:9 · Berean Standard Bible
But the LORD’s portion is His people, Jacob His allotted inheritance.
Context
7Kumbuka siku za kale;
tafakari vizazi vya zamani vilivyopita.
Uliza baba yako, naye atakuambia,
wazee wako, nao watakueleza. 8Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao,
alipogawanya wanadamu wote,
aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa
sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli. 9Kwa kuwa fungu la Bwana ni watu wake,
Yakobo kura yake ya urithi. 10Katika nchi ya jangwa alimkuta,
katika nyika tupu ivumayo upepo.
Alimhifadhi na kumtunza;
akamlinda kama mboni ya jicho lake, 11kama tai avurugaye kiota chake,
na kurukaruka juu ya makinda yake,
ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka,
na huwachukua kwenye mabawa yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.