Kumbukumbu 32:31
Deuteronomy 32:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu, sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri.
Deuteronomy 32:31 in English
Deuteronomy 32:31 · Berean Standard Bible
For their rock is not like our Rock, even our enemies concede.*
Context
29Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili,
na kutambua mwisho wao utakuwa aje! 30Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja,
au wawili kufukuza elfu kumi,
kama si kwamba Mwamba wao amewauza,
kama si kwamba Bwana amewaacha? 31Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu,
sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri. 32Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma,
na kutoka kwenye mashamba ya Gomora.
Zabibu zake zimejaa sumu,
na vishada vyake vimejaa uchungu. 33Mvinyo wao ni sumu ya nyoka,
sumu yenye kufisha ya swila.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.