Native Bible

Deuteronomy 26:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu.

Deuteronomy 26:7 in English

Deuteronomy 26:7 · Berean Standard Bible

So we called out to the LORD, the God of our fathers; and the LORD heard our voice and saw our affliction, toil, and oppression.

Context

5Kisha utatangaza mbele za Bwana Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 6Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. 7Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. 8Kwa hiyo Bwana akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. 9Akatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.