Kumbukumbu 26:6
Deuteronomy 26:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu.
Deuteronomy 26:6 in English
Deuteronomy 26:6 · Berean Standard Bible
But the Egyptians mistreated us and afflicted us, putting us to hard labor.
Context
4Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana Mungu wako. 5Kisha utatangaza mbele za Bwana Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 6Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. 7Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. 8Kwa hiyo Bwana akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.