Native Bible

Amos 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitatuma moto juu ya Yuda ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”

Amos 2:5 in English

Amos 2:5 · Berean Standard Bible

So I will send fire upon Judah to consume the citadels of Jerusalem.”

Context

3Nitamwangamiza mtawala wake na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” asema Bwana. 4Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata. 5Nitatuma moto juu ya Yuda ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.” 6Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Israeli, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Wanawauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu. 7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini, kama vile juu ya mavumbi ya nchi, na kukataa haki kwa walioonewa. Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.