Amosi 2:3
Amos 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitamwangamiza mtawala wake na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” asema Bwana.
Amos 2:3 in English
Amos 2:3 · Berean Standard Bible
I will cut off the ruler of Moab and kill all the officials with him,” says the LORD.
Context
1Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Moabu,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,
ikawa kama chokaa. 2Nitatuma moto juu ya Moabu
ambao utateketeza ngome za Keriothi.
Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa
katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta. 3Nitamwangamiza mtawala wake
na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”
asema Bwana. 4Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Yuda,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana
na hawakuzishika amri zake,
kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,
miungu ambayo babu zao waliifuata. 5Nitatuma moto juu ya Yuda
ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.