Amosi 2:6
Amos 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Israeli, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Wanawauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu.
Amos 2:6 in English
Amos 2:6 · Berean Standard Bible
This is what the LORD says: “For three transgressions of Israel, even four, I will not revoke My judgment, because they sell the righteous for silver and the needy for a pair of sandals.
Context
4Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Yuda,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana
na hawakuzishika amri zake,
kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,
miungu ambayo babu zao waliifuata. 5Nitatuma moto juu ya Yuda
ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.” 6Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Israeli,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Wanawauza wenye haki kwa fedha,
na maskini kwa jozi ya viatu. 7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,
kama vile juu ya mavumbi ya nchi,
na kukataa haki kwa walioonewa.
Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,
kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu. 8Watu hulala kando ya kila madhabahu
juu ya nguo zilizowekwa rehani.
Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo
ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.