Matendo 13:38
Acts 13:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu.
Acts 13:38 in English
Acts 13:38 · Berean Standard Bible
Therefore let it be known to you, brothers, that through Jesus the forgiveness of sins is proclaimed to you.
Context
36“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. 37Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu. 38“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. 39Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. 40Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.