Matendo 13:40
Acts 13:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate:
Acts 13:40 in English
Acts 13:40 · Berean Standard Bible
Watch out, then, that what was spoken by the prophets does not happen to you:
Context
38“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. 39Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. 40Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate: 41“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka,
mkastaajabu, mkaangamie,
kwa maana nitatenda jambo wakati wenu
ambalo hamtasadiki,
hata kama mtu akiwaambia.’ ” 42Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.