Native Bible

Acts 13:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata.

Acts 13:42 in English

Acts 13:42 · Berean Standard Bible

As Paul and Barnabas were leaving the synagogue, the people urged them to continue this message on the next Sabbath.

Context

40Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate: 41“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, mkastaajabu, mkaangamie, kwa maana nitatenda jambo wakati wenu ambalo hamtasadiki, hata kama mtu akiwaambia.’ ” 42Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. 43Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.