Matendo 13:44
Acts 13:44 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana.
Acts 13:44 in English
Acts 13:44 · Berean Standard Bible
On the following Sabbath, nearly the whole city gathered to hear the word of the Lord.
Context
42Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. 43Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana. 45Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema. 46Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.