Matendo 13:36
Acts 13:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza.
Acts 13:36 in English
Acts 13:36 · Berean Standard Bible
For when David had served God’s purpose in his own generation, he fell asleep. His body was buried with his fathers and saw decay.
Context
34Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya:
“ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika
nilizomwahidi Daudi.’ 35Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi,
“ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’ 36“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. 37Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu. 38“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.